1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya watu waliouwawa Mogadishu yaongezeka

Mohammed Abdulrahman
15 Oktoba 2018

Watu 20 wamethibitishwa kufariki na wengine 40 kujeruhiwa kufuatia shambulizi la mwisho wa juma lililopita kwenye mikahawa miwili mjini Baidoa

https://p.dw.com/p/36YNf
Somalia Gedenkveranstaltung für Opfer Anschlag vor einem Jahr
Picha: picture-alliance/dpa/F.A. Warsameh

Idadi ya watu waliouwawa katika shambulizi la miripuko miwili ya mabomu kwenye mikahawa miwili mjini Baidoa nchini Somalia mwishoni mwa juma lililopita, imefikia 20 na wengine 40 kujeruhiwa. 

Duru zimeeleza kuwa washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walijiripua katika shambulizi la mapema Jumamosi asubuhi. Kundi la  al-Shabaab limedai kuhusika na shambuliozi hilo. Msemaji wa kundi hilo amesema wameulenga mkahawa huo kwa sababu ni mahala  ambako wanajeshi huwepo kila mara.

Jumapili ilitimia mwaka mmoja, tangu shambulizi la bomu katika mji mkuu wa Somalia-Mogadishu, ambalo linashukiwa lilifanywa pia na  Al-Shabaab, lilipowauwa watu zaidi ya 500.

Mahakama ya kijeshi ya Somalia, ilimhukumu adhabu ya kifo mtu mmoja aliyekutikana na hatia  ya kuhusika katika  shambulizi hilo.