1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliouawa Algeria yaongezeka

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CazM

ALGIERS:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria,Mourad Medelci amesema,idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika mashambulizi mawili ya bomu katika mji mkuu wa Algeria,Algiers imeongezeka hadi 30.Lakini duru za hospitali zinasema hadi watu 70 wameuawa.

Mashambulizi hayo yalilenga jengo la serikali na ofisi za Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR.Miongoni mwa watu waliouawa ni wafanyakazi 11 wa Umoja wa Mataifa.Kundi la kigaidi la tawi la Al-Qaeda liitwalo Islamic Maghreb limedai kuhusika na mashambulizi hayo mawili.