1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa kwa ajali ya treni India yafikia 280

Amina Mjahid
3 Juni 2023

Idadi ya waliokufa katika ajali iliyohusisha treni tatu mashariki mwa India imependa na kufikia watu 280, na wengine karibu 900 wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4S9Xl
BG Zugunglück in Indien
Picha: Satyajit Shaw/DW

Kulingana na taarifa ya mamlaka za jimbo la Odisha ilikotokea ajali hiyo, idadi ya vifo na majeruhi inatarajiwa kuongezeka.

Uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo iliyotokea kwenye wilaya ya Balasore unaendelea ingawa sababu inaelezwa kuwa ni kutokana na treni ya abiria kuacha reli na kugongana na treni ya mizigo. Jimbo la Odisha limeitangaza Jumamosi kuwa siku ya maombolezo kutokana na mkasa huo. 

Ajali ya treni yauwa takriani watu 280 nchini

Katibu mkuu wa jimbo la Odisha Pradeep Jena, katika ujumbe wake kupitia mtandao wa twitter, amesema juhudi za uokoaji zilizofanyika Ijumaa zilihusisha zaidi ya magari 115 ya kubeba wagonjwa. Ameongeza kuwa, takribani lita 500 za damu zilikusanywa kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi wa ajali hiyo. Shughuli za uokoaji bado zinaendelea.