ICC: Mawakili wa Rais Kenyatta wataka kesi ifungwe | Matukio ya Afrika | DW | 11.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

ICC: Mawakili wa Rais Kenyatta wataka kesi ifungwe

Mawakili wa Rais Kenyatta wametaka kesi inayomkabili ifungwe kabisa kwa sababu ya mahakama imekosa ushahidi dhidi yake.

Kufuatia hatua ya mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kuwataka majaji wa mahakama hiyo kuahirisha kesi dhidi ya rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa muda usiojulikana, mawakili wa rais Kenyatta wamewataka majaji hao hao kuifunga kabisa kesi hiyo kwa sababu mahakama imekosa ushaidi dhidi ya mteja wao. Baadhi ya wachambuzi wanahoji hadhi ya mahakama hiyo itakavyokuwa ikiwa itashindwa kabisa kuendesha kesi kwa sababu ya kile inachosemwa ni kukosa ushirikiano kutoka serikali ya Kenya. Daniel Gakuba amezungumza na Bwana Ojwang Agina, mwanasheria na mchambuzi wa masuala ya mahakama hiyo, ambaye amesema kesi dhidi ya Kenyatta bado haijapotea, na ameanza kwa kutoa sababu. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za maskioni hapo chini.

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri:Yusuf Saumu

Sauti na Vidio Kuhusu Mada