1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ibada ya kumuaga Isaac Gamba yaendelea Dar es Salaam

John Juma
29 Oktoba 2018

Mamia ya waombolezaji wamekusanyika katika eneo la hospitali ya jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa mtangazaji  Isaac Gamba aliyefariki dunia Ujerumani.

https://p.dw.com/p/37IiP
Tansania Dar es Salaam - Beisetzung Isaac Gamba
Picha: DW/S. Khamis

Ibada ya kumuaga mwandishi wa habari wa idhaa ya Kiswahili DW, Isaac Muyenjwa Gamba, inaendelea Lugalo mjini Dar es Salaam.

Mamia ya waombolezaji wamekusanyika katika eneo la hospitali ya jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa mtangazaji  Isaac Gamba aliyefariki dunia Ujerumani.

Watu mbalimbali, familia, jamaa, ndugu, marafiki ,  Mkuu wa   Idhaa ya kiswahili ya DW pamoja na baadhi ya watumishi wa idhaa, waandishi wa habari wa vyombo vya kimataifa na kitaifa, wasikilizaji na waliokuwa wapendwa wa marehemu wamekusanyika eneo la hsopitali ya  Lugalo kutoa heshima zao za mwisho.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW Andrea Schmidt( kulia) mhariri wa DW Mohamed Khelef (katikati) na Naibu mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW Josephat Charo (kushoto) wakihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa Isaac Gamba
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW Andrea Schmidt(kulia) mhariri wa DW Mohamed Khelef (katikati) na Naibu mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW Josephat Charo (kushoto) wakihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa Isaac GambaPicha: DW/S. Khamis

Mwili wa Isaac Gamba uliwasili Dar es Salaam kutoka Ujerumani alfajiri ya leo.

Baadaye  mwili  wa marehemu utasafirishwa kuelekea Mwanza kisha hadi kijijini kwao Bunda kwa ajili ya mazishi ambayo  Kwa mujibu wa msemaji wa familia huenda yakafanyika Jumatano.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman