Hukumu ya kuachwa huru gaidi Brigitte MMohnhaup wa (RFA) | Magazetini | DW | 13.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Hukumu ya kuachwa huru gaidi Brigitte MMohnhaup wa (RFA)

Magazeti ya Ujerumani leo yametuwama takriban juu ya mada moja:hukumu ya kumuacha huru gaidi wa zamani wa Jeshi Jekundu la Ujerumani (RFA) Brigitte Mohnhaupt.

Baada ya kupitishiwa kifungo cha maisha korokoroni,Mohnhaupt anatazamiwa kutoka gerezani huko Bavaria, Machi 27.

Gazeti la HESSISCHE/NIEDERSÄCHSICHE ALLGEMEINE kutoka kutoka Kassel laandika:

„Nani anaemkumbuka tena Wolfgang Göbel na George Wurster ? Majina yao yamesahauliwa ,kinyume na jina la mwanamke aliesababisha vifo vyao:Brigitte Mohnhaupt,alieongoza makamando wa April,7,1977 kumuua mshtaki mkuu wa serikali Siegfried Buback na washirika wake- dereva George Wurster na Wolfgang Göbel.

Kwa jamaa zao siku ya kuachwa kwake huru Brigitte itakua siku ngumu,juu ya hivyo hakuna cha kukosoa hukumu iliotolewa na Mahkama kuu ya Bavaria.

Ama gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU lina hakika kwamba, kuwahusu magaidi wa jeshi Jekundu la RFA,dola inatoa ishara ya pili:kwamba chini ya msingi ya utu wa mwanadamu na sheria ndio ilipompitishia wakati ule hukumu ile.Na kwa bahati mbaya miaka 30 nyuma sawa na katika vita vya kupambana na ugaidi katika karne ya 3 baadhi ya nyakati ilitumia nguvu kupita kiasi na kuwanyima raia uhuru wao na kufanya binafsi dola litiliwe shaka.

Kwamba sasa dola hili linamtendea Bibi Brigitte Maunhaupt sawa na mhalifu mwengine pia ni ishara njema.Kwa jamaa wa wahanga kuachwa kwake huru kunavumilika kwa sharti kwamba, nje ya gereza aweza kufanya kile hakufanya akiwa gerezani:kutoa matamshi wazi ya kuomba kujuta aliyoyatenda.

Hata katika WIESBADENER KURIER mhariri ana yakini kwamba kwa kuachwa huru gaidi la zamani Brigitte Maunhaupt baada ya kutumika kifungo chake cha lazima ,hakimu alifuata barabara muongozo wa kisheria.Yaweza kutegemewa kwamba kwa magaidi wengine waliobakia korokoroni kama Christian Klar,Eva Sybille Haule na Brigit Hogenfeld ifikapo mwaka 2009 na 2011 nao pia watasamehewa .Huu ni utaratibu wa kisheria unaowafanya magaidi wa zamani kutowafanya mashahidi wala kuwakirimu hadhi za wafungwa wa kisiasa.

Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE kutoka Erfurt laandika:

„wanavyofanyiwa magaidi wa Jeshi Jekundu kwa dola linalofuata sheria kunasalia kuwa swali la imani.Mahkama haiwezi kujikomboa kutoka shaka shaka kwamba inashawishika kisiasa….. Rais wa Ujerumani anakabiliwa kwahivyo na chaguo gumu.

Ama kwa jicho la gazeti la NORDBAYERISCHER KURIER linalochapishwa mjini Bayreuth mkasa huu uko wazi:

Laandika:

„Bibi Brigitte Manahaupt akiachwa huru,hicho kitakua kibao katika uso wa watu ambao hadi leo wanateseka kwa kuuliwa na RAF jamaa zao…. Kuachwa huru kwa bibi Mohnhaupt kisheria yamkini ni sawa, hata hivyo, uzito wa kitendo alichofanya unaacha dosari kwa mahkama.

Likitumalizia gazeti la MAIN-ECHO kutoka Aschaffenburg lasema kuwa patashika iliozuka kuhusu kauchwa huru kwa Brigitte Mohnhaupt sawa na kule kunakosubirfiwa kwa Christan Klar ambako rais wa Ujerumani Horst Kohler anakuzingatia kihisia kunaeleweka ,kisheria lakini hakuna hoja.Kwani, Mohnhaupt si gaidi la kwanza kuachwsa huru na mapema na Klar si wa kwanza kwamba atasamehewa.Wametumika vifungo vyao.Na maishani mwao watakereka kiadilifu na dhulma waliotenda.Hawataweza kujisafisha na dhumla hiyo;na hakuna yeyete atakaweza kuwakomboa na maovu waliotenda.