1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hujuma za Martin dhidi ya Merkel na kiu cha T.May magazetini

Oumilkheir Hamidou
27 Juni 2017

Hujuma za Martin Schulz dhidi ya kansela Angela Merkel na makubaliano ya kuundwa serikali ya wachache nchini Uingereza ndio mada mbili kuu magazetini .

https://p.dw.com/p/2fSIS
Deutschland SPD Programmparteitag in Dortmund
Picha: picture alliance/dpa/J. Güttler

Tunaanzia lakini Ujerumani ambako kampeni za uchaguzi mkuu zimepamba moto miezi  takriban mitatu kabla ya siku ya siku kuwadia. Kilichohanikiza zaidi lakini magazetini ni hujuma za mgombea wa kiti cha kansela kutoka chama Social Democrats Martin Schulz jumapili iliyopita mjini Dortmund, dhidi ya kansela  Angela Merkel. Martin Schulz alimkaripia kansela akisema mbinu zake za kukaa kimya ni kinyume na demokrasia. Kuna wahariri wanaokubaliana na hoja hizo na wengine wanaozikosoa. Mhariri wa gazeti la "Rhein-Zeitung" anahisi kampeni za uchaguzi mwaka huu zitakuwa za malumbano". Gazeti linaendelea kuandika. "Kutokana na hali ya mambo ndani ya chama cha Social Democrat  na jinsi inavyoashiria ndani  ya vyama ndugu vya Christian Democratic Union na Christian Social Union -CDU/CSU, tunaweza kusema tutashuhudia kampeni  za malumbano makali mwaka huu.

 

Wanasocial Democrat kawaida wanawawakilisha watu wenye mapato ya chini na ya wastani, huku vyama ndugu vya CDU/CSU wakiwawakilisha wale wenye mapato ya wastani na ya juu. Inamaanisha malumbano kuhusu yaliyomo katika sera za kampeni za uchaguzi yatakuwa makali kupita kiasi katika kipindi cha miezi mitatu inayokuja. Ili kuyafikia malengo yao lakini, hakuna anaestahiki kumsingizia mwenzake hafuati demokrasia.

 

Gazeti la "Saarbrücker Zeitung" linaandika: "CDU/CSU wangefanya vyema kama hawatojiachia kunasa katika mtego waliowekewa na Martin Schulz. Anahitaji uangalifu ili kuwafikishia ujumbe wake wapiga kura. Na tuhuma zake dhidi ya Markel zina ukweli ndani yake na hilo CDU/CSU wanalitambua. Kwa miaka kadhaa sasa wanafuata mkakati ambao lengo sio kujipatia wapiga kura zaidi bali kuwachochea wale wa  upande wa upinzani kusalia majumbani....Kwamba hali hiyo haisaidii kuimarisha demokrasia, hakuna asotambua.

Biashara isiyokuwa na tija ya Theresa May

Mada yetu ya mwisho magazetini inatufikisha Uingereza ambako waziri mkuu Theresa May amefanikiwa kufikia maridhiano  pamoja na chama cha Ireland Kaskazini kinachopigania kuendelea eneo hilo kuwa sehemu ya Uingereza-DUP. Ni sawa na biashara, linaandika gazeti la "Landeszeitung". "Maridhiano hayo pamoja na DUP yatamgharimu Theresa May Euro bilioni moja nukta saba. Fedha hizo, washirika hao wepya wanataka zitumike kwa sehemu kubwa kugharimia miundo mbinu. Mtu anaweza kuzungumzia mbinu za kununua sauti na sio za kuunda serikali ya wachache. Waziri mkuu wa Uingereza hataki kujua  biashara hiyo amefungiana na nani. Muhimu kwake anaendelea kusalia madarakani Downing Street nambari kumi, kwa msaada wa DUP. Pindi mpango wa kujitoa Uingereza katika Umoja wa ulaya Brexit ukikamilika, mpaka wa nje wa Umoja wa ulaya utabidi kuwekwa kati ya jamhuri ya Ireland na sehemu ya Ireland ya kaskazini-hali itakayosababisha mvutano katika eneo hlo. Hatimae bei May atakayolazimika kulipia itakuwa kubwa zaidi kuliko ile waliyokubaliana.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri