1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hillary Clinton yamshinda Obama

9 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cmxu

MANCHESTER-MAREKANI:

Seneta wa Marekani Hillary Clinton ameshinda kura za awali za jimbo la New Hampshire kwa tiketi ya chama cha Demokrats.

Ushindi huu umekuja baada ya siku moja tu ambapo kura ya maoni ilionyesha kuwa mpinzani wake Baraka Obama angepata ushindi.Na katika upande wa chama cha Republicans,Seneta John McCain amemshinda mpinzani wake –Gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney pamoja na mshindi wa kura za Iowa- Mike Huckabee.Senetor MacCain,mwenye umri wa miaka 71,amefufua kampeini zake juzi baada ya kufifia katika kipindi cha kiangazi.Na katika chama cha Demokrats, kambi ya Hillary Clinton imeweza kujizoazoa na kushinda mpambano kwa karibu sana dhidi ya Obama wa asili mia tatu. Siku tano zilizopita,Clinton alishika nafasi ya tatu katika kura za Iowa. Mgombania mwingine wa Demokrats- John Edwards ameshika nafasi ya tatu lakini aamesema taendelea kupambana licha ya kuwa nyuma ya Clinton na Obama.