Hillary Clinton na Barack Obama kupambana Pennsylvania leo | Habari za Ulimwengu | DW | 22.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Hillary Clinton na Barack Obama kupambana Pennsylvania leo

-

WASHINGTON

Wagombea wa chama cha Demokratic Hillary Clinton na Barack Obama wanapambana tena hii leo katika uchaguzi wa awali wa kumtafuta mgombea wa chama hicho atakayegombea urais katika uchaguzi wa rais nchini Marekani mnamo mwezi Novemba.

Uchaguzi wa awali katika jimbo la Pennsylvania ni muhimu na hasa kwa bibi Hillary Clinton ambaye anabidi kupata ushindi mkubwa ili aweze kuendelea na kampeini zake za kuwania kuingia ikulu. Kumekuweko na shinikizo zaidi kutoka kwa wakuu wa chama cha Demoktatic za kutaka bibi Clinton aachie ngazi na kutoa nafasi kwa Barack Obama ambaye anaongoza kwa idadi ya wajumbe wanaomuunga mkono kuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu.

Katika miezi ya hivi karibuni wagombea hao wawili wa chama cha Demokratic wamekuwa wakilumbana hali ambayo inaonekana kumpa nguvu mgombea wa chama cha Republican John McCain za kujipigia Debe.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com