Hilary Clinton ateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya kigeni | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Hilary Clinton ateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya kigeni

Rais Mteule wa Marekani Barack Obama ametangaza kikosi cha masuala ya usalama na kumemteua mpinzani wake wa zamani Bi Hilary Clinton kuwa Waziri wa mambo ya kigeni nchini humo.

Rais Mteule Barack Obama amtambulisha Hilary Clinton kama Waziri wa mambo ya kigeni mteule

Rais Mteule Barack Obama amtambulisha Hilary Clinton kama Waziri wa mambo ya kigeni mteuleChini ya mpango huo Waziri wa Ulinzi Robert Gates anaendelea kushika wadhifa huo.

Bi Clinton na Bwana Obama wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu masuala ya sera za kigeni na ulinzi nchini humo ila kwa sasa watashirikiana kubadili sura ya Marekani katika nchi za kigeni vilevile usimamizi katika vita kwenye mataifa ya Iraq na Afghanistan.

Rais mteule Barack Obama alipuuza tofauti zao na kusisitiza anaunga mkono mjadala katika kikosi chake kipya na kumsifu Bi Clinton.


Bwana Obama alisisitiza kuwa ana imani vikosi vya Marekani vitaondoka nchini Iraq katika kipindi cha miezi 16 punde baada ya kuapishwa.Hata hivyo alieleza kuwa atashauriana na wadau wakuu kuhusu suala hilo.Kadhalika Bwana Obama aliwateua Jenerali mstaafu James Jones kuwa mshauri mkuu wa kitaifa na Gavana wa Arizona Janet Napolitano kuwa mkuu wa idara ya usalama wa kitaifa.


Afisa wa masuala ya kisheria wa zamani Eric Holder naye ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu na Susan Rice aliyekuwa mshauri wa masuala ya kigeni ameteuliwa kuwa balozi katika Umoja wa mataifa.Wadhifa huo umepangwa kuorodheshwa katika Baraza la Mawaziri.


Wateule hao wanasubiri kuidhinishwa na Baraza la wawakilishi,Senate bila pingamizi zozote.

DW inapendekeza

 • Tarehe 02.12.2008
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G7IG
 • Tarehe 02.12.2008
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G7IG
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com