HELSINKI.Waziri mkuu wa Israel atakiwa ajieleze | Habari za Ulimwengu | DW | 13.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HELSINKI.Waziri mkuu wa Israel atakiwa ajieleze

Finland ambayo inashikilia uwenyekiti wa sasa wa nchi za umoja wa ulaya imemtaka waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert kueleza zaidi juu matamshi yake kuhusu silaha za nyuklia.

Bwana Olmert amezusha kelele nchini mwake wakati alipoashiria kuwa Israel inamiliki silaha za nyuklia alipofanya mahojiano na televisheni ya hapa Ujerumani.

Waziri wa ulinzi wa Finland Seppo Kaariainen amesaema kwamba Umoja wa Ulaya utaangalia kwa makini jinsi nchi za mashariki ya kati zitakavyo yapokea matamshi hayo ya waziri mkuu wa Israel.

Bwana Olmert kwa sasa yuko njiani kuelekea Roma nchini Italia kwa mazungumzo na waziri mkuu Romano Prodi na baba mtakatifu Benedikt wa 16.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com