1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Helmut Schmidt afariki dunia

Admin.WagnerD10 Novemba 2015

Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Schmidt akitambulika zaidi kwa mapambano yake nchini mwake dhidi ya ugaidi katika miaka ya 1970 amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 96.

https://p.dw.com/p/1H3az
Deutschland Altkanzler Helmut Schmidt auf Intensivstation
Kansela wa zamani wa Ujerumani magharibi Helmut SchmidtPicha: picture alliance/Geisler-Fotopress

Helmut Schmidt kansela wa iliyokuwa Ujerumani magharibi kuanzia 1974 hadi 1982 alitangazwa kuwa amefariki Jumanne mchana.

Kansela huyo wa iliyokuwa Ujerumani magharibi ya zamani Helmut Schmidt , ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa miaka minane mnamo wakati wa kipindi cha vita baridi, amefariki akiwa na umri wa miaka 96, imesema ofisi yake mjini Hamburg jana Jumanne.

Schmidt alikuwa kansela wa pili wa chama cha siasa za wasitani za mrengo wa shoto cha Social Democratic SPD katika Ujerumani magharibi kuanzia 1974 hadi 1982 na mwanaharakati mkubwa wa kupigania umoja wa Ulaya.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kwamba Schmidt alipatwa na maambukizi baada ya upasuaji kuondoa damu iliyoganda katika mshipa katika mguu wake kiasi ya miezi miwili iliyopita.

Deutschland Helmut Schmidt Alt-Bundeskanzler
Helmut Schmidt katika mijadala ya vipindi vya mazungumzoPicha: Getty Images/P. Lux

Mzee wa taifa

Katika miaka ya hivi karibuni, Schmidt , ambaye alikuwa akivuta sigara nyingi kwa siku, akilikuwa mgeni wa mara kwa mara katika vipindi vya mazungumzo na alikuwa akiheshimika zaidi kama mzee wa taifa kuliko wakati alipokuwa akiliongoza taifa hilo.

"Nimesikitishwa mno na kifo cha Helmut Schmidt. Alikuwa kansela aliyefanyakazi yake vizuri, kifo chake ni pigo kwa Ujerumani na Ulaya, spika wa bunge la Ulaya Martin Schulz kutoka chama cha Social Democratic ameandika katika ukurasa wa Tweeter.

Waziri wa fedha wa serikali ya Ujerumani Wolfgang Schäuble CDU, amesema Ujerumani imepotelewa na mtu muhimu. Akiwa kama meya wa jiji la Hamburg , waziri wa fedha na kansela wa Ujerumani, Helmut Schmidt alitambua kuwa hili litatokea. Alipata nguvu kupambana katika wakati wa mizozo.

Mwenyekiti wa chama cha SPD na makamu kansela wa Ujerumani Sigmar Gabriel amesema tumo katika msiba mkubwa kwa kifo cha Helmut Schmidt na tunajivunia kwamba alikuwa mmoja wetu. Uwezo wake wa maamuzi na ushauri tutaukosa.

Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker , amemueleza Schmidt kuwa ni rafiki, ambaye mimi binafsi pamoja na bara zima la Ulaya tutamkosa .

Kwasababu tumempoteza mtu muhimu, ambaye ameweza kuonesha nguvu zake kisiasa.

Deutschland Helmut Schmidt Alt-Bundeskanzler
Hemut SchmidtPicha: picture-alliance/dpa/W. Kumm

Muumini wa Umoja wa Ulaya

Helmut Schmidt ameonesha uwezo mkubwa wa kipekee, uwezo wa kuangalia hali ya baadaye. Uwezo huu ni ushahidi kwetu , ambao hatutaweza kuutupa, tukiangalia bara la Ulaya.

Mkuu wa kundi la wabunge wa chama cha SPD bungeni Thomas Oppermann, nae ameeleza kwamba anajisikia wivu kuhusiana na maisha aliyoendesha Helmut Schmidt. Alikuwa muumini halisi wa siasa za Social democratic na Ulaya iliyoungana.

Mwenyekiti wa chama cha kijani Cem Özdemir amesema tunaomboleza kifo cha Helmut Schmidt na tutakosa umahiri wake, ucheshi na mapambano yake ya kisiasa, na vitendo.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amekuwa mmoja kati ya marais waliotangulia kutoa rambirambi zao kwa kusema kiongozi muhimu katika bara la Ulaya ametutoka. Hollande amesema Schmidt alikuwa mzalendo halisi na mtu muhimu katika taifa la Ujerumani, ambaye kila wakati alitia hamasa katika mijadala . "Kila mara alisema ni lazima kuruhusu uchumi wa soko kuwapo, lakini ni lazima kuupa mtazamo wa kijamii".

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman