HEILIGENDAMM: Maafikiano kupambana na ongezeko la ujoto duniani | Habari za Ulimwengu | DW | 08.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HEILIGENDAMM: Maafikiano kupambana na ongezeko la ujoto duniani

Viongozi wa madola manane tajiri yalioendelea kiviwanda G-8,wameafikiana njia za kupambana na ongezeko la ujoto duniani.Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anaeongoza mkutano wa viongozi hao mjini Heiligendamm,kaskazini mwa Ujerumani, ameyasifu makubaliano hayo kama ni “mafanikio makubwa.”Akaongezea kuwa makubaliano hayo yatasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa,gesi zinazochafua mazingira na ni hatua muhimu kuelekea lengo la kupunguza gesi hizo kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2050.Maafikiano hayo lakini hayakupanga ratiba ya malengo au kiwango maalum.Kwa upande mwingine,wanasiasa wa Chama cha Kijani cha Ujerumani wamemkosoa Kansela Merkel kuwa ameachana na madai yake mwenyewe na matakwa ya baadhi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com