1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Heiligendamm. Boti za polisi na waandamanaji wa Greenpeace zagongana.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtv

Boti za polisi zikiwa zinalinda maeneo ya maji kuzunguka eneo la mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri duniani G8 , zimegonga boti mbili za kujaza upepo ambazo zimekiuka eneo la usalama la mkutano huo.

Wanaharakati wa ulinzi wa mazingira wa Greenpiece, wamesema kuwa walikuwa wanakimbizana na polisi wakati tukio hilo lilipotokea.

Polisi wamesema waandamanaji watatu na afisa wa polisi wamejeruhiwa na kwamba maboti yote yamepelekwa katika bandari ya karibu.

Kwa upande wa waandamanaji walioko nchi kavu, maelfu ya waandamanaji wameendelea kuweka vizuizi katika njia kuelekea katika mkutano huo, na mamia ya watu wengine wamejikusanya kuzunguka uzio wa umbali wa kilometa 12 uliowekwa kwa ajili ya usalama.

Wakati huo huo tamasha la muziki dhidi ya kundi la G8 katika mji wa karibu wa Rostock limeanza ambapo mwanamuziki wa kundi la U2 , Bono anatarajiwa kushiriki pamoja na Bob Geldof.