1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILGENDAMM: Pendekezo la Rais Putin linavutia

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBto

Rais George W.Bush wa Marekani amesema,pendekezo la kuwa na mpango wa pamoja wa makombora ya kinga nchini Azerbaijan,linavutia.Hapo awali,Rais Vladimir Putin wa Urusi alipozungumza na Bush kando ya mkutano wa kilele wa G-8 mjini Heiligendamm alisema,hatua ya kwanza ya mpango huo ni kutumia pamoja rada za Urusi,ambazo tayari zipo nchini Azerbaijan.Vile vile akasema, ameshazungumza na rais wa Azerbaijan kuhusu suala hilo.Bush kwa upande wake amesema,atalifikiria pendekezo hilo.Kabla ya mkutano wa kilele wa G-8, serikali ya Moscow ilipinga vikali mpango wa Marekani wa kutaka kuweka makombora yake ya kinga nchini Poland na Jamhuri ya Czech.