HAVANA:Rais wa Angola akutana na Castro mwishoni mwa ziara yake nchini Cuba | Habari za Ulimwengu | DW | 24.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HAVANA:Rais wa Angola akutana na Castro mwishoni mwa ziara yake nchini Cuba

Rais Jose Eduardo dos Santos wa Angola amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Cuba kwa kukutana na Fidel Castro ambapo nchi hizo mbili zimetiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano.

Rais wa muda wa Cuba Raul Castro ambaye alimwalika kiongozi huyo wa Angola alisema kuwa ziara hiyo imeyakinisha uhusiano mzuri na wakidugu kati ya nchi hizo mbili.

Magazeti ya Cuba yalichapisha picha zinazomuonesha Rais Dos Santos akiwa na Fidel Casro.

Mapema televisheni ya Cuba ilionesha mahojiano na kiongozi huyo anayeumwa ambapo alizungumzia mambo kadhaa yakiwemo kuimarika kwa thamani ya fedha ya Euro dhidi ya dola.

Hatua hiyo ni katika kukanusha uvumi ya kwamba kiongozi huyo wa Cuba amefariki au hali yake ni mbaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com