HAVANA:Cuba yamlaumu Bush, na kumuita mhalifu | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HAVANA:Cuba yamlaumu Bush, na kumuita mhalifu

Cuba imemlaumu Rais George Bush wa Marekani na kumuita mhalifu asiye na mamlaka ya kufidisha uadilifu, kufuatia hotuba yake hapo jana kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa iliyotaka kuwepo kwa uchaguzi wa kidemokrasia nchini Cuba.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba iliyotolewa mjini Havana imemlaumu Rais Bush kwa kuwatesa wafungwa katika jela ya Guantanamo Bay.

Imesema kuwa kiongozi huyo wa Marekani hana mamlaka wala sifa za kuweza kuhukumu nchi nyingine.

Rais Bush katika hotuba yake hapo jana alisema kuwa utawala aliyouita wa kidikteta wa muda mrefu nchini Cuba unakaribia mwisho wake na kwamba wananchi wa nchi hiyo wako tayari kwa uhuru wao.

Matamshi hayo yaliufanya ujumbe wa Cuba kwenye mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kutoka nje.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com