Havana. Sherehe za malizika bila Castro kujitokeza. | Habari za Ulimwengu | DW | 03.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Havana. Sherehe za malizika bila Castro kujitokeza.

Wiki moja ya sherehe za heshima kwa rais wa Cuba Fdel Castro zimemalizika bila ya mwenyewe kutokeza hadharani.

Kutokuonekana kwake kunaonekana kuwa ni ishara kuwa Castro bado hajapata nafuu kutokana na upasuaji aliofanyiwa hapo mwezi Julai.

Mamia kwa maelfu ya watu walikuwa mjini Havana kwa ajili ya sherehe hizo ambazo zinaadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi huyo na miaka 50 ya siku ambayo Castro pamoja na waasi nchini Cuban walipoanzisha mapinduzi katika kisiwa hicho.

Akizungumza mwishoni mwa gwaride la kijeshi la kufunga sherehe hizo, kaimu rais na mdogo wake rais Fidel Castro, Raul castro, amesisitiza nia ya serikali ya kisiwa hicho kutaka mazungumzo na Marekani yenye lengo la kumaliza miongo kadha ya vikwazo vya kibiashara vya Marekani dhidi ya Cuba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com