1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA: Fidel Castro akaribia kupona.

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvZ

Rais wa Cuba, Fidel Castro anakaribia kupata nafuu kabisa kutokana na upasuaji wa utumbo wake aliofanyiwa mwaka uliopita.

Taarifa hiyo imetolewa na rais wa bunge Ricardo Alarcon ambaye pia anashikilia nafasi ya tatu miongoni mwa viongozi walio na ushawishi mkubwa nchini humo.

Hata hivyo Ricardo Alarcon hakusema iwapo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka themanini atarejea kwenye wadhifa wa urais.

Fidel Castro hajaonekana hadharani tangu tarehe 31 mwezi Julai mwaka uliopita alipomkabidhi madaraka mdogo wake Raul Castro.