1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA : Castro kurudi kazini karibuni

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNN

Kiongozi wa Cuba Fidel Castro kwa mara ya kwanza amejitokeza katika matangazo ya moja kwa moja tokea augue hapo mwezi wa Julai.

Kiongozi huyo mgonjwa mwenye umri wa miaka 80 akizungumza hewani moja kwa moja na Rais Hugo Chavez wa Venezuela katika kipindi cha radio na amesema alikuwa akijihisi kuwa na nguvu zaidi. Waziri wa mambo ya nje wa Cuba Felipe Perez Roque amesema wakati akiwa ziarani nchini Honduras hapo jana kwamba Fidel Castro anaweza kurudi kazini hivi karibuni.Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa afisa yoyote yule wa serikali ya Cuba kugusia juu ya uwezekano wa kiongozi huyo wa Cuba kurudi ofisini.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Cuba ameliwacha wazi suala la iwapo au la Castro yumkini akarudi katika serikali kwa kiasi fulani na kumwachia kaka yake mwenye umri wa miaka 75 Raul Castro ambaye ni waziri wa ulinzi aendelee kuongoza nchi.