Hatma ya Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini kufuatia mvutano wa kisiasa na Jacob Zuma | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.09.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hatma ya Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini kufuatia mvutano wa kisiasa na Jacob Zuma

mNchini Afrika Kusini mvutano wa kisiasa kati ya Rais Thabo Mbeki na Jacob Zuma kiongozi wa chama tawala cha African National Congress ANC umechukua sura mpya.

default

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini

Baraza la mawaziri nchini humo linasubiri uamuzi wa chama hicho tawala kuhusu hatma ya Rais Mbeki kufuatia mvutano huo.Wiki iliyopita mahakama ilitupilia mbali kesi ya ufisadi na ubakaji iliyomkabili Bwana Jacob Zuma.Yote hayo yamezua tetesi kuwa Rais Mbeki huenda akajiuzulu kabla ya muhula wake kukamilika.Itakumbukwa kuwa Bwana Zuma alitoa kauli iliyosisitiza kuwa ni muhimu kwa Rais Mbeki kumaliza muhula wake.

Ili kupata picha kamili Thelma Mwadzaya amezungumza na Isaac Nkomo mwandishi wa habari mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com