Hatimaye matumaini ya kuokolewa. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 09.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Hatimaye matumaini ya kuokolewa.

Wachimba migodi nchini Chile wafikiwa na mtaimbo maalum.

default

Ishara ya Maria mtakatifu inayotoa matumaini kwa wachimba migodi 33 walionaswa chini ya ardhi nchini Chile.

SAN JOSE:

Wachimba migodi 33 walionaswa chini ya mgodi sasa wamefikiwa na mtaimbo.

Mtaimbo huo ulichimba na kuingia katika sehemu waliponaswa wafanyakazi hao umbali wa futi alfu mbili chini ya ardhi. Na sasa itawezekana kutengeneza upenyo utakaowezesha kuteremsha kitasa maalumu kitakachowapakia watu hao na kuwafikisha juu ya ardhi. Mlio wa king'ora ulioashiria kufaulu kwa juhudi za kuwafikia wachimba migodi hao uliwapa faraja watu hao pamoja na ndugu zao nchini Chile kote.

Rais Sebastian Pinera wa Chile amesema, kile ambacho kingeliweza kuwa msiba sasa kimegeuka kuwa neema.Watu hao sasa wanatarajiwa kuuona tena mwanga wa jua katika muda wa siku chache zijazo.

 • Tarehe 09.10.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PaEl
 • Tarehe 09.10.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PaEl
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com