Hatimaye kampuni ya Canada yashinda: | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hatimaye kampuni ya Canada yashinda:

Kampuni ya Canada, Magna International italinunua tawi la General Motors-Opel la nchini Ujerumani.

default

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefurahia uamuzi wa General Motors.

Bodi  ya wakurugenzi ya  kampuni  ya magari ya Marekani  Generel Motors imeamua kuliuza tawi lake la Ujerumani,Opel kwa kampuni ya Canada ,Magna  International.

Kansela  wa  Ujerumani Angela Merkel amethibitisha uamuzi  huo  aliokuwa anaupendelea  wakati  wote. 

Akizungumza  na waandishi habari mjini Berlin Kansela  Merkel alithibitisha  uamuzi wa bodi ya wakurugenzi  wa  kampuni  ya General Motors. Kiongozi   huyo wa Ujerumani  amefurahishwa na  uamuzi  huo.

Uamuzi wa bodi hiyo unamaliza hali ya wasiwasi iliyokuwa inawakabili  wafanyakazi 25,000 wa tawi la Opel  la Ujerumani. 

Serikali  ya Ujerumani wakati wote imekuwa inaiunga mkono  kampuni  ya  Canada Magna International  na imesema itatenga kiasi cha Euro bilioni 4 .5  kama dhamana  ya kuisaidia kampuni hiyo   katika  juhudi  za kuleta muundo mpya kwenye  tawi.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anaamini kuwa pendekezo hilo litakubalika kwa General Motors.

Kampuni ya GM imesema  itadumisha asilimia 35 ya hisa  na itauza asilimia 55  kwa kampuni ya hiyo ya Magna.  Wafanyakazi watamikili asilimia 10 katika  kile General Motors ilichoita Opel mpya.

Mwandishi:Meyer-Feist,Andreas/Wien (ARD)

Mtafsiri:A.Mtullya

MhaririM.Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com