1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimaye Al-Shabbaab waruhusu misaada ya kibinaadamu Somalia

18 Julai 2011

Baada ya miaka miwili ya kuyazuwia mashirika ya misaada yasihudumu ndani ya ardhi ya Somalia, hatimaye wanamgambo wa Al-Shabbaab wameyaruhusu kwa mara ya kwanza mashirika hayo kuyafikia maeneo yanayokabiliwa na njaa.

https://p.dw.com/p/11yN5
Wakimbizi wa Kisomali wakipatiwa msaada katika kambi ya Dadaab, Kenya.
Wakimbizi wa Kisomali wakipatiwa msaada katika kambi ya Dadaab, Kenya.Picha: Picture-Alliance/dpa

Kwa ujumla, hali katika eneo la Pembe ya Afrika inaripotiwa kuwa mbaya kwa sababu ya ukame na uhaba mkubwa wa chakula unaowalazimisha maelfu ya raia wa Somalia na Ethiopia kuingia katika nchi jirani ya Kenya, hasa katika kambi ya Dadaab iliyo kaskazini mwa nchi hiyo, kutafuta nusura.

Kwa mara ya kwanza, ikiwa ni baada ya miaka miwili, Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF) limefanikiwa kupeleka shehena ya chakula kwenye eneo la kusini mwa Somalia, baada ya wanamgambo wa Al-Shabbaab kukubali mashirika ya kibinaadamu kuanza kutoa huduma zake kwenye maeneo yanayoshikiliwa na kundi hilo.

Thelma Mwadzaya amezungumza na msemaji wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) aliyeko kwenye kambi ya Dadaab, Kaskazini mwa Kenya, Rose Ogola, juu ya huduma ambazo wakimbizi hupatiwa wanapovuuka mpaka na kuingia Kenya.

Mahojiano: Thelma Mwadzaya/Rose Ogola
Mhariri: Othman Miraji