Hatima ya kocha wa Ufaransa leo | Michezo | DW | 02.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hatima ya kocha wa Ufaransa leo

Hatima ya Raymond Dominique kama kocha wa Ufaransa itajulikana leo.

Leo Julai 3, hatima ya kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa-makamo bingwa wa dunia Raymond Dominique itajulikana iwapo atasalia kiti au la. Stadi wa Urusi katika kombe la Ulaya Andrei Arshavin asema ataka kuihama klabu yake mabingwa wa kombe la ulaya la UEFA Zenit St.Petersberg.Kisa nini ?

Na bingwa wa dunia wa mbio za masafa ya mita 100 na 200 Muamerika Tyson Gay ameanza kujinoa kwa changamoto na wajamaica Usain Bolt na Asafa Powell.

Hatima ya kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa-makamo bingwa wa dunia itajulikana leo baada ya Ufaransa kupigwa kumbo na mapema nje ya kombe la ulaya.

Dominique kabla ya kikao cha leo ameungwamkono aendelee kuwa kocha tangu na nahodha wa Ufaransa Patrick Vieira,stadi Franck Ribery

Kuna wengine lakini, wanahisi Raymond Dominique wakati wake wa kun'gatuka umefika.Miongoni mwao ni nahodha wa zamani Zinedine Zedane alieiongoza Ufaransa kutwaa kombe la dunia 1998.

Zidane anampendekeza Didier Deschamps ashike wadhifa huo.Dominique ambae mkataba wake unadumu hadi kombe la dunia 2010 nchini Afrika Kusini,anakabili hii leo Baraza la shirikisho la dimba la Ufaransa (FFF) kupima mafanikio ya timu chini yake.

Wajumbe 21 wa Baraza hilo litajadiliana kabla mwenyekiti wake Jean-Pierre Escalettes kutangaza uamuzi katika mkutano wa waandishi habari mchana wa leo.

Stadi wa Urusi katika kombe lililopita la Ulaya Andrei Arshavin amesema anataka kuiachamkono klabu yake ya Zenit St.Petersberg -mabingwa wa kombe la UEFA la Ulaya.

Alisema kwamba angependa kujiunga na klabu nyengine.

Arshavin alinawiri katika kombe la Ulaya na kumekuwapo klabu kadhaa zilizoonesha hamu ya kumuajiri.Inasemekana FC barcelona ya Spian imepiga hodi kwa Zenit.Arshavin mwenye umri wa miaka 27 ni mchezaji bora wa mwaka wa Russia,alitamba pale Russia ilipoitimua nje ya kombe la ulaya Holland.

Michezo ya olimpik ya beijing ikinyemelea, wanariadha kila pembe ya dunia, wanajinoa kwa michezo hiyo:

Bingwa wa dunia wa masafa ya mita 100 na 200,muamerika Tyson Gay ameeleza anatumai kujinoa zaidi kwa Olimpik kwa kukimbia muda bora katika mita 100 akipambana uso kwa uso na mjamaica Asafa Powell, bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia kutoka Jamaica.

Changamoto yao inatazamiwa katika mashindano ya baadae mwezi huu ya Grand Prix mjini London.Tayson Gay alikimbia muda bora kabisa aliponyakua tiketi yake ya kuiwakilisha Marekani hivi majuzi.Muda wake ulikuwa sek.9.68 lakini ulisaidiwa na upepo na haikutambuliwa kuwa rekodi.Asafa Powell aliweka rekodi ya sek. 9.74 iliodumu hadi mwezi mei, mwaka huu pale mjamaica mwengine ilipofutwa na Usain bolt wa Jamaica.

Changamoto kati ya Powell na Gay inatazamiwa kwahivyo, kuzaa rekodi mpya ya dunia .