Hatima ya gereza la Guantanamo | Magazetini | DW | 23.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Hatima ya gereza la Guantanamo

Guantanamo na Zimbabwe ni mada kuu 2 zilizochambuliwa na wahariri.

(President Robert Mugabe ZANU PF's )

(President Robert Mugabe ZANU PF's )

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo yamechambua mada mbali mbali kuanzia hali ya uchumi itakavyokuwa mwaka mpya,kuhusu Kanzela wa zamani Helmut Schmidt,rais-mteule Barack Obama na gereza la Guantanamo,Zimbabwe na Mugabe hadi uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano wa vyama vya mrengo wa shoto-SPD na Link Partei.

Ramadhan ali anaanza gazeti la Westdeutsche Zeitung (West-doech)na kisa cha gereza la Guantanamo ambamo wafungwa wanaotuhumiwa ugaidi na utawala wa George Bush wamewekwa:

"Ikiwa uaminifu ni kutimiza ahadi anazotoa mwanasiasa,waziri wa nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier bora angenyamaza kimya.Kwani, ni waziri huyu wa nje aliejitolea kwa rais-mteule Barack Obama, kuwapokea Ujerumani wale wafungwa wa Guantanamo wasio na hatia.Imesadifu ni waziri huyu huyu Steinmeier,akiwa waziri katika afisi ya Kanzela aliekataa kumrejesha Murat Kurnaz nyumbani ujerumani ingawa wamarekani hawakumuamngalia tena Murat ni gaidi la kiislamu.

Ikiwa sasa mtetezi huyu wa wadhifa wa ukanzela wa chama cha SPD anataka kusahau hayo,basi afadhali kuhusu mkasa wa Guantanao afunge mdomo."

Likiendeleza mada hii hii,gazeti la Sudwest Presse ) laandika:

"Rais -mteule Barrack Obama tayari wakati wa kampeni ya uchaguzi kuwa anataka kuifanya Marekani nchi inayopalilia uhuru na haki za binadamu.Kwa kushika usukani huo wa kiadilifu,hawezi tena kuvumilia gereza la Guantanamo.Bila shaka mtu awetza kutoa hoja kwamba ni jukumu la wamarekani kuumaliza mzozo juu ya Guantanamo.Lakini,kufuatia mkasa wa shambulio la kigaidi la Septemba 11 ,haitawezekana kwa rais wa Marekani kuthubutu hivyo........

Ni busara kwa nchi za ulaya ili kuambatana na kanuni zake kutoikatalia Marekani,zisije kuikatalia Marekani msaada na kuzuwia kufungwa kwa gereza la Guantanamo.Jukumu hilo pia inalo Ujerumani.Ujerumani katika kuonesha mshikamano yapaswa kumsaidia Obama ili kulifuta kabisa doa la Guantanamo."

Likitugeuzia mada ,gazeti la Schwabische Zeitung"

linadaia kuwa,kila mahala wananchi wanadai vikosi vya Ujerumani virejeshwe nyumbani kutoka Afghanistan na hata kwa mshirika wa chanda na pete-Uingereza.Gazeti laongeza:

"Marekani inazingatia sasa vita kuvieneza hadi nchini Pakistan.

Kuna hatari ya kuvikuza vita wakati mtu wa kawaida nchini Afghanistan hana usalama wake binafsi na wanalalamika juu ya rushua katika utawala wasioupenda wa Karsai."

Kuhusu rais Mugabe wa Zimbabwe na kungangania kwake madaraka,gazeti la Braunschweiger Zeitung- laandika:

Rais Mugabe amegeuka kutoka kiongozi aliewekewa matumaini kwa afrika bora na kuwa alielichimbia kaburi bara la Afrika.Ameiapiza Afrika.Katika uchu wake wa madaraka ,amewakaripia majirani ambao nao ni woga kumuondoa madarakani. Maradhi ya kolera hayapo tena ,yameshaondoshwa.Maradhi hayo kwa muujibu wa rais Mugabe yalikuwa propaganda tu kuipa Marekani kisingizio kutekeleza mpango wake ilioundaa zamani wa kujiingiza kijeshi.

Gazeti linauliza:

"Je, ulimwengu uipe kisogo zimbabwe huku wananchi wake wanakufa na njaa au wanateseka kwa maradhi ?Ulimwengu ufumbe macho huku wafungwa wakiteswa kinyama kabisa-wanajeshi watoto kama huko Mashariki mwa Kongo wanaua kutoka kijiji kimoja hadi kingine na wakati nchi za kiafrika kwa woga wao na kwa ubinafsi wao zinatumbua macho tu ?

Maswali haya yanahitaji majibu ."