Hatari ya kutoweka kwa aina za mbegu, kutokana na udhibiti wa makampuni makubwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hatari ya kutoweka kwa aina za mbegu, kutokana na udhibiti wa makampuni makubwa

Tumo katika hali ya mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanasababisha hali mbaya ya hewa yenye kuharibu mazao. Tunahitaji mbegu zinazohimili ukame ili kulisha jamii inayoongezeka.

default

Kampuni kubwa la kuzalisha mbegu bora la monsanto.

Tumo katika hali ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuwa na hali ya hewa mbaya ambayo pia inaharibu mazao. Mazao, ambayo tunayahitaji sana, ili kuweza kuilisha jamii ya watu wanaoongezeka kwa kasi. Jibu linaweza kuwa ni kupatikana aina ya mimea ya mazao ambayo inaweza kuhimili mabadiliko haya ya hali ya hewa. Lakini kuweza kukuza mazao haya , tunahitaji pia utamaduni wa kuwa na aina nyingi ya mimea kama hiyo tofauti. Mfumo wa soko, hata hivyo, unaelekeza kwa aina chache tu.

Kwa zaidi ya karne kadha wakulima wamekuwa wakilima mazao. Mavuno ya mwaka mmoja huwa mazuri, kwa miaka kadha wakipanda mimea mchanganyiko katika mashamba yao, na kufanikiwa kupata mavuno mazuri kwa mazao hayo tofauti kwa matumizi yao mbali mbali. Hii leo soko la bidhaa duniani linamilikiwa na makampuni machache makubwa. Makampuni matatu yanadhibiti asilimia 47 ya soko lote la chakula. Kile kinachofahamika kama mbegu zinazozalishwa kwa wingi ambazo zinafanyiwa biashara na makampuni hayo, hazitumiwi na wakulima hawa wa kawaida, ama kufanyiwa kilimo mchanganyino. Aina hii ya mbegu kutoka kwa makampuni haya inatishia kuondoa kabisa aina ya mbegu za asili.

Athari zaidi ya uzalishaji huu wa zao moja ni kwamba aina nyingine za mbegu zimo katika hatari ya kupotea. Kwa sababu tukiangalia, ni aina ngapi za mbegu zipo kwa mahindi, kwa viazi, samaki na kadhalika, tunaona kuwa ni muhimu namna gani kuiendeleza hali hii anuai, ili kuweza kupata uwezekano wa kuendeleza maisha.

Anasisitiza Manfred Niekisch, mkurugenzi wa bustani ya wanyama mjini Frankfurt, na mwanachama wa baraza la wataalamu wa masuala ya hali ya hewa. Umuhimu wa uhai anuai kwa upande wa mbegu za asili na wanyama ni mkubwa. Watafiti wanatahadharisha juu ya kutawala kwa mbegu ya aina moja tu, kwa sababu vinasaba katika mbegu vikipotea , vitakuwa vimepotea daima. Na pia anatahadharisha Manfred Niekisch, kwamba hatufahamu ni lini tutavihitaji tena.

Kujenga uwezo kwa mfano wa kuhimili magonjwa, ama dhidi ya ukame, ama dhidi ya unyevunyevu, unaoleta aina ya uyoga , na vitu vingine. Ukulima wa zao moja kwa hiyo utapunguzwa ili kupata mbegu nyingi zaidi, ama wanyama wengi zaidi, na hii ni muhimu sana , iwapo tutafikiria kuhusu mageuzi ya maendeleo ya maisha hapa duniani.

Wakati huo huo, katika nchi nyingi kuna wanaharakati ambao wanapinga kilimo hiki cha zao moja. Mbinu za hivi sasa za kupata vinasaba na makampuni ya mbegu kama Monsanto, kwa mfano, si tu kwamba yanapigwa vita katika maeneo kama India , lakini hata nchini Marekani kwenyewe , ambako kilimo cha mbegu kama hizo kinachofanywa na kampuni hilo kubwa linaloongoza katika siko la dunia kinapigwa vita. Kwa kweli, anasema Benedikt Haerlin kutoka wakfu wa mapango wa kilimo cha hapo baadaye nchini Ujerumani, kwamba watu wengi zaidi wanajiuliza kuhusu hali ya baadaye ya kilimo, kwa jumla.

Tunapaswa kujiuliza sana iwapo kilimo ambacho huzalisha chakula kidogo kwa matumizi ya watu, kitaweza kukidhi mahitaji ya viwanda ambayo yanazidi kukua. Na watu wengi hata hapa Ujerumani, Marekani, bara lote la Ulaya , Australia, Japan wanajiuliza na kusema utaratibu huu ni mbovu.

Ni utaratibu mbovu, anasema Haerlin, kwamba karibu nusu ya ardhi ya kilimo ni kwa ajili ya chakula cha wanyama pamoja na mbegu kwa ajili ya nishati , kuhusu matumizi ya nyama na kuendesha magari katika mataifa tajiri. Kwa wakulima umuhimu wa kilimo hicho ni kujipatia fedha, ambazo hawakuwa wanazihitaji hapo kabla. Kwa wakulima wengi hali hii haileti tu kitisho cha njaa. lakini kinawaelekeza katika kuathirika mapato yao.

Mwandishi: Helle Jeppesen/ Kitojo, Sekione/ZR

Mhariri: Miraji Othman

:

E N D E

 • Tarehe 15.06.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NrJ3
 • Tarehe 15.06.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NrJ3

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com