Hatari ya kipindupindu kwa raia wa Congo walioikimbia Goma | Matukio ya Afrika | DW | 31.05.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Hatari ya kipindupindu kwa raia wa Congo walioikimbia Goma

Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF, limeonya kuwa mamia ya maelfu ya watu waliokimbia mji wa Goma nchini DRC, kufuatia mlipuko wa volcano wanakabiliwa na hatari ya maambuzi ya ugonjwa wa kipundupindu

Baada ya volcano ya mlima Nyiragongo kuunguruma wiki moja iliyopita, hofu ya kutoka kwa mlipuko wa pili imeilaazimu serikali kutoka amri ya kuondolewa watu siku ya Alhamisi, ambayo ilishuhudia wakaazi laki nne wakiyakimbia makaazi yao.

Karibu robo yao walikimbilia Sake, karibu kilomita 30 Kaskazini-Magharibi, wakati wengine wakielekea Rutschuru katika upande wa kaskazini, na Minova, katika mkoa wa Kivu Kusini.

Soma zaidi: Goma yakabiliwa na uhaba wa chakula baada ya volkano

Katika kijiji cha Sake, MSF imekuwa ikipambana na mlipuko wa kipindupindu kwa miaka kadhaa sasa, na kati ya watu laki moja na laki moja na themani wamechukua hifadhi huko, na kuongezea kwenye idadi ya wakaazi wake wapatao elfu 70.

Rais Felix Tshisekedi amewataka waathirika kusubiri kurejea makwao

DR Kongo | Präsident Félix Tshisekedi in Kinshasa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Felix Tshisekedi

Rais Felix Tshisekedi  amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuachana kwa sasa na mawazo  ya kurejea kwao jijini Goma kama inavyo takiwa na baadhi yao kutokana na uhaba wa vyakula na maji safi.

Akiuhutubia mkutano wa wanahabari mwishoni mwa juma lililo pita huko kinshasa, Tshisekedi amedai kuwa serikali imeanza kuwahudumia hivi sasa maelfu ya waliokimbilia Sake.

soma zaidi:Watu waachwa bila makaazi kufuatia tetemeko la ardhi Rubavu

Hata hivyo, baadhi ikiwa ni wanawake na watoto wanao songamana katika jengo la shule lililojengwa kwa mbao, ombi lao ni chakula na maji safi ambavyo bado kuwasili hapa licha ya tangazo lililo tolewa naye rais mwishoni mwa juma.

Shirika la huduma za kiutu la Umoja wa Mataifa OCHA, limesema baada ya mlipuko zaidi ya nyumba 4,500 iliharibiwa na lava, na kuathiri karibu watu elfu 20. Ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, umeanza ufuatiliaji wa angani wa volcano hiyo.

Mwnadishi: Benjamin Kasembe