Harusi ya Mwanamfalme William na Kate wa Uingereza | Masuala ya Jamii | DW | 29.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Harusi ya Mwanamfalme William na Kate wa Uingereza

Ni Rasmi, Mwanamfalme William na mpenzi wake, Katherine ni mke na mume. Wawili hao walizifunga pingu zao za maisha mapema hii leo katika kanisa kuu la Westminster Abbey lililo katikati ya mji wa London.

default

Mwanamfalme William akimbusu mkewe Kate Middleton katika kasri la Buckingham

Mamilioni ya watu walilishuhudia tukio hilo la kihistoria kwenye eneo lililo karibu na kanisa, kadhalika kwenye televisheni. Muda mfupi baada ya kuozwa, Mwana mfalme William alimbusu mkewe Kate Middleton waliposimama kwenye roshani ya Kasri la Buckingham wakati ndege za kijeshi zilipopuruka angani kwa heshima ya Mwanamfalme William. Ili kupata picha halisi ya mambo yalivyokwenda Thelma Mwadzaya alizungumza na Suleiman Salim, mkaazi wa jiji la London wa muda mrefu na mwandishi wa habari...


Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com