Harris kutangaza jina la mgombea mwenza wa umakamu wa rais
5 Agosti 2024Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Kamala Harris anatarajiwa hii leo kumtaja mgombea mwenza atakayewania nafasi ya umakamu wa rais, wakati akijiandaa kwa ziara yake katika majimbo yenye ushindani mkubwa nchini humo.
Harris ataanza ziara yake ya siku tano katika jimbo kubwa la Pennsylvania siku ya Jumanne ili kutafuta uungwaji mkono wa kudumu unaoweza kumwezesha kushinda uchaguzi wa Novemba. Tangazo la mgombea mwenza anatarajiwa kulitoa kabla ya mkutano wa hadhara wa Jumanne huko Philadelphia. Kamala Harris aashiria mabadiliko makubwa kwenye sera ya Marekani kuhusu Gaza.
Baadaye wiki hii, Harris atazuru Sun Belt na majimbo ya kusini mwa Arizona, Nevada, Georgia na North Carolina, huku akitafuta kura za Wamarekani weusi na jamii ya Wahispania.
Harris ambaye ni mwendesha mashtaka wa zamani amevunja rekodi za uchangishaji fedha, kuvutia umati mkubwa wa watu na kutawala mitandao ya kijamii.