1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare: Wanaharakati wa upinzani waachiwa huru

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPl

Polisi nchini Zimbabwe imewaachia huru wanaharakati 32 wa upinzani waliokamatwa wakati maafisa wa usalama walipouvunja mkutano wa hadhara wa ulioitishwa na kiongozi mkuu wa upinzani Morgan Tsvangirai Jumapili iliopita. Watu wote 33 waliachiliwa huru baada ya kulipa faini ya dola 2,500 za Zimbabwe sawa na dola 10 za kimarekani. Kwa miaka mitano sasa polisi imekua ikizuwia mikutano mikubwa ya upinzani na kuwatia nguvuni waandalizi.

Chama cha Movement for Democratic Change-MDC, kimepanga kuanzisha vuguvugu jipya la upinzani kabla ya uchaguzi wa rais mwaka ujao. Hata hivyo uchaguzi huo unakabiliwa na kitisho, baada ya wafuasi wa chama tawala ZANU-PF cha Rais Mugabe kuunga mkono muda wake urefushwe hadi 2010, ili uchaguzi huo ufanyike sambamba na ule wa bunge. Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika bunge la sasa linalodhibitiwa na ZANU-PF , ili kuidhinishwa.