1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare. Operesheni punguza bei yaendelea.

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBka

Polisi wa Zimbabwe wamewakamata zaidi ya wamiliki 1,300 wa maduka na wakuu wa biashara kwa kwenda kinyume na amri ya serikali ya kupunguza bei.

Radio ya taifa hilo imesema leo kuwa serikali ya rais Robert Gabriel Mugabe , ikiwa na wasi wasi juu ya kupanda mno kwa bei hali ambayo inaweza kuleta ghasia katika jamii, iliamuru maduka na biashara kadha kupunguza bei za bidhaa zao hadi katika kiwango ambacho kilitumika Juni 18, ama watakabiliwa na hatua ya kukamatwa.

Wiki iliyopita wachunguzi wa bei wakifuatana na polisi walianza kutembelea maduka nchini kote wakiamuru kupunguza bei, baadhi ya nyakati hata kwa nusu chini msako wa polisi uliopewa jina la operesheni punguza bei.