HARARE : Mugabe apongeza utiifu wa wanajeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 15.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HARARE : Mugabe apongeza utiifu wa wanajeshi

Rais Robert Mugabe amepongeza utiifu wa vikosi vyake vya ulinzi na kuwashutumu wapinzani kwa kujaribu kuzidisha mateso ya kiuchumi na ameapa kudumisha utulivu nchini Zimbabwe.

Mugabe ambaye alikuwa akihutubia katika gwaride la kijeshi kuadhimisha Siku ya Majeshi inayoadhimishwa kila mwaka kwa mara nyengine tena hapo jana amewashutumu wapinzani wa serikali kwa kuhusika na kupanda kwa bei za bidhaa kwa kusema kwamba wao na vikwazo vya mataifa ya magharibi wamekusudia kuyafanya maisha nchini Zimbabwe yazidi kuwa magumu sana.

Agizo la serikali la kupunguza bei kwa bidhaa zote na huduma kwa karibu nusu hapo mwezi wa Juni kumepelekea kuwepo kwa uhaba mkubwa wa unga wa mahindi,mkate,nyama,mafuta ya petroli na bidhaa nyengine muhimu nchini Zimbabwe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com