1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Hofu kuwa Tsvangirai amevunjwa fuvu

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJ2

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe,Morgan Tsvangirai anapokea matibabu katika kitengo cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum,ikidhaniwa kuwa amevunjika fuvu.Tsvangirai alipigwa kikatili na polisi baada ya kukamatwa siku ya Jumapili pamoja na wanaharakati darzeni kadhaa walipohudhuria mkutano wa kuipinga serikali.Leo asubuhi,alishindwa kufika mahakamani kwa sababu ya hali yake mbaya.Tsvangirai ameapa kuendelea kumpinga Rais Robert Mugabe.Uchumi wa Zimbabwe umezorota vibaya sana,chini ya utawala wa Mugabe. Kiasi ya watu milioni 3.5 wameikimbia Zimbabwe kutafuta kazi nchi za ngámbo.Mfumuko wa bei wa kila mwaka,sasa ni asilimia 1,700 na ukosefu wa ajira ni kama asilimia 80.Wakati huo huo,umri wa wastani wa mtu kuishi nchini Zimbabwe,ni miaka 37,ukiwa ni umri mdogo kabisa kote duniani.