HANOI:Mazungumzo kati ya Japan na Korea Kaskazini yavunjika ghafla | Habari za Ulimwengu | DW | 08.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HANOI:Mazungumzo kati ya Japan na Korea Kaskazini yavunjika ghafla

Mazungumzo ya kurejesha uhusiano kati ya Japan na Korea Kaskazini, yamevunjika. Mapema bila ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote.

Mazungumzo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi, hayakuchukua zaidi ya saa moja kabla ya kuvunjika huku kukiwa hakuna tarehe yoyote iliyopangwa kwa mazungumzo mengine.

Maafisa wa pande zote mbili wamekuwa wakilaumina kwa kushindwa kukubaliana katika masuala muhimu..

Hii ni mara ya pili mazungumzo hayo kuvunjika ambapo hapo siku ya jumatato mazungumzo hayo yalivunjika ghafla.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com