Hannover, Ujerumani. Maonyesho yafunguliwa rasmi. | Habari za Ulimwengu | DW | 15.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Hannover, Ujerumani. Maonyesho yafunguliwa rasmi.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefungua rasmi maonyesho ya kila mwaka ya kibiashara ya masuala ya komputa na mawasiliano yanayojulikana kama CEBIT.

Vifaa vya kisasa kabisa vitaonyeshwa katika maonyesho hayo makubwa ya aina yake , wakati simu za mkononi, teknolojia ya digital na uunganishaji katika mtandao wa internet kwa haraka vinatarajiwa kuwavutia watu wengi watakaotembelea.

Maonyesho ya Cebit yawavutia waonyeshaji bidhaa zaidi ya 6,000 kutoka mataifa 77 katika muda wa wiki moja, lakini maonyesho hayo yameshindwa kuweka hali ya mvuto wake ilioupata wakati wa biashara ya mtandao wa Internet ilipoanza.

Katika maelezo yake wakati wa ufunguzi, Merkel amesema ataitisha mkutano wa masuala ya mawasiliano nchini Ujerumani baadaye mwaka huu ili kuweka pamoja rasilmali za sayansi, viwanda na siasa ili kupambana na changamoto za hapo baadaye.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com