Hamilton akaribia kutetea ubingwa wa dunia | Michezo | DW | 12.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hamilton akaribia kutetea ubingwa wa dunia

Bingwa wa sasa wa dunia wa mbio za magari ya Formula One Lewis Hamilton anakaribia kuhifadhi taji lake na kushinda ubingwa wa tatu wa dunia baada ya ushindi wake katika mbio za Russia Grand Prix

Lakini timu yake ya Mercedes tayari imeweka jicho moja katika msimu wa 2016 baada ya kuthibitishwa kuwa mabingwa wa taji la ujenzi kwa mwaka wa pili mfululizo.

Muingereza Hamilton sasa anaongoza msimamo wa madereva akiwa na pointi 302 mbele ya Sebastian Vettel wa Ferrari ambaye ana pointi 236 naye Nico Rosberg wa Mercedes akiwa na 229.

Ushindi wa jana ulikuwa wa 42 kwa Hamilton katika Formula One na kumpiku gwiji wa mashindano hayo Aryton Senna.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga