Hamburg yamtimua kocha wake | Michezo | DW | 23.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Hamburg yamtimua kocha wake

Klabu ya Hamburg inayokabiliwa na kitisho cha kushushwa daraja imemtimua kocha wake kwa mara ya pili msimu huu baada ya Joe Zinnbauer kupigwa kalamu kufuatia matokeo duni

Mkurugenzi wa michezo Peter Knaebel amechukua usukani wa kuliokoa jahazi la timu hiyo ya Bundesliga.

Knaebel, ni kocha wa tatu kuiongoza Hamburg msimu huu baada ya Zinnbauer aliyechukua nafasi ya Mirko Slomka, aliyepigwa kalamu mwezi Septemba..

Hamburg waliponea kwenye tundu la sindano kushushwa daraja msimu uliopita baada ya kutoka sare mikondo yote miwili ya michuano ya mchujo na Greuther Fuerth na kubakia katika ligi kuu kwa faida ya goli la ugenini.

Zinnbauer ni kocha wa saba katika Bundesliga kufutwa kazi msimu huu baada ya Robin Dutt wa Werder Bremen, Slomka, Jens Keller wa Schalke 04, Armin Veh wa Stuttgart, Kasper Hjulmand wa Mainz na Jos Luhukay wa Hertha Berlin.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: AbdulRahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com