1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Steinmeier akutana na wapatanishi wa Iran

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cd

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amekutana na wapatanishi wawili wa Iran wanaoshughulikia mgogoro wa nyuklia wa Iran. Kwa mujibu wa duru za Ujerumani,Steinmeier alitoa mwito kwa mpatanishi mpya wa Iran,Said Jalili na mtangulizi wake Ali Larijani kujaribu kuwa na majadiliano ya ushirikiano pamoja na mkuu wa Shirika la Nishati ya nyuklia la Umoja wa Mataifa Mohamed El-Baradei na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana.