Hamas yahitaji kuangalia mapendekezo ya Israel | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 24.12.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Hamas yahitaji kuangalia mapendekezo ya Israel

Kundi hilo la Hamas linasubiri kupitia mapendekezo hayo katika kufikiwa makubaliano ya kuachiwa wafungwa wa Kipalestina na mwanajeshi wa Israel.

default

Wafuasi wa Hamas katika maadhimisho ya miaka 22 tangu kuanzishwa kundi hilo, zilizofanyika Gaza Desemba 14, 2009

Kiongozi wa kundi la Hamas, Mahmoud al-Sahar amesema atahitaji siku kadhaa kuangalia mwitikio wa Israel katika pendekezo lake la kubadilishana wafungwa wa Kipalestina na mwanajeshi wa Israel anayeshikiliwa na kundi hilo.

Radio ya Israel imeripoti kuwa mpatanishi wa Ujerumani amewasilisha nyaraka kwa wawakilishi wa Hamas huko Gaza, ambapo pia alifanya mazungumzo na wawakilishi hao.

Kundi la Hamas linataka kuachiwa huru kiasi Wapalestina 1,000 ili kubadilishana na mwanajeshi huyo, Gilad Shalit anayeshikiliwa na kundi hilo kwa miaka mitatu na nusu sasa.

Awali Israel ilitoa masharti kuwa zaidi ya wafungwa 100 inayowaona ni hatari sana, hawataruhusiwa kwenda katika Ukingo wa Magharibi, lakini watapelekwa tu Gaza au nje ya nchi.

 • Tarehe 24.12.2009
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/LCh6
 • Tarehe 24.12.2009
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/LCh6
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com