HALLE: Wazee 13 wamefariki katika ajali ya basi | Habari za Ulimwengu | DW | 19.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HALLE: Wazee 13 wamefariki katika ajali ya basi

Ajali ya basi iliyotokea jimbo la Sachsen-Anhalt,mashariki mwa Ujerumani imeua abiria wazee 13 na kuwajeruhi wengine 31,wengi wao wakiwa katika hali ya mahututi.Kwa mujibu wa polisi,lori moja liligonga basi hilo upande wa nyuma na kulisukuma bondeni.Basi hilo lilikuwa na abiria 49 waliotokea jimbo la North Rhine Westphalia na walikuwa njiani kwenda mapumzikoni mji wa Dresden mashariki ya Ujerumani.Hii ni ajali mbaya kabisa ya basi kupata kutokea nchini Ujerumani tangu mwaka 1992.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com