Hali yarejea kawaida Thailand | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 03.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Hali yarejea kawaida Thailand

Waandamanaji wanaopinga serikali nchini Thailand wameondoka kwenye viwanja viwili vikuu vya ndege mjini Bangkok baada ya kuvizingira tangu wiki iliyopita

Waandamanaji wa chama cha People's Alliance for Democracy,PAD wakisherehekea ushindi wao

Waandamanaji wa chama cha People's Alliance for Democracy,PAD wakisherehekea ushindi wao


Ushindi wao huo umefanikishwa na uamuzi wa mahakama ya katiba uliomlazimisha Waziri mkuu Somchai Wongsawat kujizulu.Kwa sasa viongozi waliongolewa madarakani wanakutana kujadili hatua ya kumteua kiongozi wa muda nchini humo.


Kiongozi wa upinzani wa chama cha Democratik nchini humo Appisyed Vechasiwat anasisitiza kuwa nchi hiyo inahitaji uongozi bora


Suala tete linalosubiri ufumbuzi ni atakayekuwa madarakani nchini Thailand kwa sasa baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu jambo ambalo huenda likazua ghasia zilizo na misingi ya kisiasa.


Hata hivyo chama cha Peoples Alliance for Democracy PAD kimetisha kusababisha vurugu endapo madai yao hayatotimizwa.


Kwa upande mwingine msemaji wa Shirika la Ndege la kitaifa la Thai Airways Ajcharnaporn na Songhkla amesema kuwa ndege ya kwanza ya abiria itaondoka saa nane mchana za Thailand ikitokea kisiwani Phuket.Ndege hiyo itatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa SuvarnabhumiDW inapendekeza

 • Tarehe 03.12.2008
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G86T
 • Tarehe 03.12.2008
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G86T
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com