1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya watoto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni mbaya sana

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfjr

KINSHASA:

Shirika lisilo la kiserikali la Okoa watoto, linasema kuwa hali ya watoto mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imefikia kiwango cha maafa.

Wapiganaji kutoka upande wote wanawatumia watoto kama ngao,amesema Hussein Murshal,mkurugenzi wa kundi hilo la kimataifa la kutoa misaada nchini kongo.

Mapigano katika jimbo lenye matatizo la mashariki yameongezeka kwa kiwango kikubwa tangu mwezi wa agosti, wakati makundi hasimu ya waasi yakipigana katika maeneo ya msitu.