Wizara ya Afya visiwani Zanzibar leo imetangaza wagonjwa wapya saba wa virusi vya corona, huku ikiwa ni siku ya nne Tanzania Bara haijatoa taarifa yoyote kuhusu ugonjwa huo.
Ili kufahamu hali ilivyo kwa sasa, Grace Kabogo amezungumza na afisa wa programu ya elimu ya afya kwa umma katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania, Dokta Tumaini Haonga ambaye pia ni mmoja wa wajumbe katika timu ya wataalamu ya kupambana na COVID-19 nchini humo. Sikiliza