Hali ya uchaguzi nchini Kenya | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Hali ya uchaguzi nchini Kenya

Taasisi tatu tofauti nchini Kenya zimefanya kura ya maoni kuhusu uchaguzi ujao na kubainisha kuwa kiongozi wa ODM Bwana Raila Odinga anaongoza akifuatiwa na rais Mwai Kibaki wa chama cha PNU.

Chama hicho kilizindua kampeni zake rasmi hapo jana katika uwanja wa michezo ya Nyayo huku chama cha ODM kikinyimwa ruhusa ya kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Uhuru. Hata hivyo bunge bado halijavunjwa ila kiongozi wa taifa hilo anatangaza kuwa uchaguzi utafanyika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Mwandishi wetu Mwai Gikonyo ana taarifa kamili kutoka Nairobi.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com