1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya mashariki ya kati

Oumilkher Hamidou29 Desemba 2008

Dhamiri za hujuma eti kweli ni uchaguzi mkuu ujao nchini Israel?

https://p.dw.com/p/GObt
jela yahujumiwa na wafungwa wakimbia GazaPicha: AP



Mbali na mada kuhusiana na fuko la huduma za afya na miito ya kupunguza kodi za mapato,wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamechambua kwa mapana na marefu hali ya mashariki ya kati kufuatia hujuma za jeshi la Israel katika Gaza.


Passauer Neue Presse linaandika.


"Jicho kwa jicho,jino kwa jino,ukipiga nitapiga na kisasi kwa kisasi na kila wakati,kila upande unadai una haki ya kujihami.Katika wakati ambapo pande hizi mbili hazitaweza kulizima janga la jahannam,amani itasalia kua ndoto tuu katika ardhi takatifu.Na hali hii bila ya shaka, wanaitambua tangu serikali ya Israel na pia viongozi wa utawala wa ndani wa Palastina walioko Ukingo wa Magharibi,katika wakati ambapo Hamas wanaolidhibiti eneo la Gaza,hawataki hata kidogo kusikia.Wanataka vita vya maangamizi dhidi ya Israel.Ndio maana ingekua bora kama wapalastina wenyewe wangepiga kura dhidi ya Hamas.Hapo matumaini yangeweza kupata nguvu kwamba pengine rais mpya wa Marekani,Barack Obama angeupa msukumo utaratibu wa amani ya mashariki ya kati.


Gazeti la Münchner Merkur linahisi maguvu yote haya ya kijeshi yamelengwa uchaguzi mkuu ujao nchini Israel.Gazeti linaendelea kuandika:


"Hujuma za kijeshi za Israel dhidi ya Gaza zimesababishwa na ile hali kwamba uchaguzi mkuu unakurubia kuitishwa nchini Israel na hakuna hata upande mmoja ulio tayari kumuachia adui mkubwa wa Israel akiyatia hatarini maisha ya raia wa nchi hiyo.Olmert na Livni wamezongwa na kizungumkuti:hawataki kuwaachia wafuasi wa siasa kali,hawataki pia kuwaachia wapiga kura waangukie mikononi mwa mkakamavu asietaka suluhu Benjamin Netanyahu.Kuendesha vita dhidi ya Hamas lakini inamaanisha pia,kutumbukia katika mtego wa kisaikolojia wa adui-Picha za televisheni zimeonyesha nyumba zinazowaka moto na maiti za raia wa kawaida wasiokua na hatia.Hamas hawajajificha bure katika maeneo ya karibu na mahala wanakoishi wakinamama na watoto wasiokua na hatia."


Mada yetu ya pili magazetini inahusu fuko la kugharimia huduma za afya.Gazeti la Augsburger Allgemeine linaandika:


"Hatulitakii mema fuko la aafya tunapodai kwamba ughali wa vitu unatokana zaidi na uamuzi wa wanasiasa wa kutenga mabilioni ya yuro kwaajili ya mishahara ya madaktari na kugharimia vyombo vya kimambo leo vya hospitali.Kwa maneno mengine bila ya fuko la afya mashirika ya bima ya afya yangelazimika kwa mara nyengine tena mwaka huu kusawazisha viwango vya malipo,ikimaanisha kupandisha viwango hivyo.


Gazeti la Wiesbadener Kurier linaandika:


"Wajuaji wameshaanza kufikiria njia gani itakua bora na ambayo mwisho itawaangukia walipa kodi tuu.Kabla ya kutwikwa mzigo mwengine ,kila upande miongoni mwa wahusika wa mfumo wa afya utabidi uwajibike:hesabu zichunguzwe,gharama zidhibitiwe na wagonjwa nao pia wawajibike.