1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya kisiasa katika chama cha CCM nchini Tanzania

15 Oktoba 2009

<p>Chama cha Mapinduzi CCM nchini Tanzania kimesema kinakusudia kuzika hali ya uhasama inayoendelea kujitokeza sasa baina ya wabunge wa chama hicho kabla hata ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

https://p.dw.com/p/K73h
Kwani kama hali hiyo itaendelea kuwepo, inaweza kupoteza umaarufu wa chama hicho na pengine kuvuruga kabisa uchaguzi wenyewe. Hayo yalisemwa hii leo na Naibu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa wakati akisoma ripoti ya kamati ya uchunguzi ya chama hicho juu ya uhasama uliozuka kati ya makundi tofauti ya wanasiasa wa chama hicho.

Mwandishi wetu kutoka Dar es Salaam, George Njogopa ametutumia taarifa ifuatayo:

Mwandishi: George Njogopa

Mtayarishaji: Grace Patricia Kabogo

Mhariri: M.Abdul-Rahman