1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Hatari huenda ikatangazwa nchini Pakistan

9 Agosti 2007

Rais Parves Musharaf wa Pakistan huenda akatangaza hali ya hatari ambayo itadhibiti shughuli za mahakama za nchi hiyo, harakati za kutetea haki za kiraia na uhuru wa vyombo vya habari.

https://p.dw.com/p/CB25
Jenerali Parves Musharaf rais wa Pakistan
Jenerali Parves Musharaf rais wa PakistanPicha: PA/dpa

Vyombo vya habari vimeripoti kuhusu mazungumzo baina ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice na rais Musharaf mapema leo juu ya hatua hiyo ya kutangaza hali ya hatari nchini Pakistan.

Wakati huo huo rais Musharaf ameghairi safari yake ya kwenda nchini Afghanistan kuhudhuria mazungumzo ya kikabila yanayolenga kutafuta mkakati wa kuangamiza uasi wa kundi la Taliban.

Rais Musharaf badala yake amemteua waziri wake mkuu Shaukat Aziz kuihudhuria kikao hicho.

Hakuna sababu zozote zilizotolewa juu ya uamuzi huo war ais Musharaf wa kughairi kuhudhuria mkutano huo uliopangwa kuwakutanisha pamoja na rais Hamid Karzai wa Afghanistan, wazee wa kikabila na maafisa wa Marekani.

Wizara ya mambo ya nje ya Afghanistan imesema kwamba kutohudhuria mazungumzo hayo rais Parvez Mushara hakuta athiri mipangilio.