Hali tete kwa wanawake nchini Iraq | Masuala ya Jamii | DW | 06.11.2006
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Hali tete kwa wanawake nchini Iraq

Hali ya wanawake nchini Iraq bado ni mbaya katika jamii kwasababu ya vita kati ya makundi ya kidini vinavyohatarisha maisha ya wanawake.

Wanawake wa Iraq

Wanawake wa Iraq

Katiba nchini humo inaagiza kwamba wanawake wote sharti wafuate sheria za dini yoyote ile wanayofata.Yanar Mohammed ni kiongozi wa Shirika la Kutetea haki za wanawake na uhuru nchini Iraq.

Kwa sasa maswala ya wanawake yanapuuzwa katika mazingira ya vita kati ya makundi ya kidini japo idadi ya wanawake wanaopoteza maisha yao kwasababu ya ghasia inazidi.Wengi wanasema kwamba wanahofia maisha yao hata shughuli kama kwenda kazini zinawatatiza.

Wapiganaji waliojihami kwa silaha hutokea wakati wowote hata katika mabasi ya abiria na kuagiza watu kulala chini ili wamsake wanayemtafuta kwa sababu zao.Wapiganaji hao wanalipiza kisasi kwa kuwashambulia wanawake wa upande wanaopambana nao.Hiki ni kipindi kigumu kwa wakazi wa Iraq kwani utawala huu umeondoa uhuru wa wanawake uliokuwako katika sheria ya kijamii ya awali.

Shirika hilo la kutetea uhuru wa wanawake linashughulika hasa na maswala ya kutafuta msaada wa kuimarisha hali ya wanawake ikiwemo pia mipango ya kuanzisha taasisi ya habari na mawasiliano ,Al Arabic al Musasawat.Kulingana na Yanar Mohammed wanawaanda wanawake kwa mafunzo ya kuweza kujieleza katika jamii.

Kadhalika tuna kitengo cha kuwasimamia wanawake walioteswa jela au hata mahali pa kujistiri panapotokea mateso kwani kuna visa vingi vimeripotiwa vya unyanyasaji wawanawake.Mbali na hayo tunawahusisha vijana katika maswala ya kitamaduni anasema kiongozi huyo.

Kundi hilo linazongwa na matatizo ya fedha vilevile usalama duni unaohatarisha maisha yao.Hivi karibuni balozi wa Marekani nchini Iraq Zalmay Khalilzad alisema kuwa Iraq inaweza kujisimamia baada ya mwaka mmoja u nusu.Kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo hadhani kwamba wanafahamu hali halisi ya mambo nchini Iraq.

Ghasia zinazidi na wanaona kama huo ni uongo mtupu.Aidha hadhani kwamba jamii ya kimataifa ina imani na wanayosema kwani kila walichotaja hakijafanikiwa.Tunaona kama wanatupuuza na kutuchezea akili na hatutaki kuyasikia anamaliza Bi Yana Mohammed.

 • Tarehe 06.11.2006
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHmB
 • Tarehe 06.11.2006
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHmB
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com