1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali nchini Rwanda

Oumilkher Hamidou16 Mei 2010

Matumizi ya nguvu yanazidi miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa rais nchini Rwanda

https://p.dw.com/p/NPL4
Rais Paul Kagame wa RwandaPicha: picture-alliance/ dpa

Mtu mmoja ameuwawa na wengine 28 kujeruhiwa jana usiku baada ya bomu la mkono kufyetuliwa katika mtaa wa kibiashara wa mji mkuu wa Rwanda-Nyabugogo,mjini Kigali.

Hilo ni shambulio la tatu katika kipindi cha miezi mitatu kufanywa katika eneo hilo hilo linalotembelewa na watu wengi mjini Kigali.

Mashambulio matatu yameshatokea,tangu february 19 katika eneo hilo linalolindwa vikali na vikosi vya usalama nchini Rwanda.Jumla ya watu watatu wamepoteza maisha yao na wengine wasiopungua 50 kujeruhiwa.Hakuna aliyedai kuhusika na mashambulio hayo.Polisi wameahidi kuwasaka na kuwakamata wahusika.

Mashambulio haya yanatokea katika wakati ambapo Rwanda inajiandaa kuitisha uchaguzi wa rais Agosti tisaa mwaka huu.Rais Paul Kagame ameshachaguliwa na chama chake cha Patriotic Front kutetea wadhifa wake.

Mandishi :Hamidou Oummilkheir

Imepitiwa na :Ramadhan Ali